Kulingana na Shirika la Habari la ABNA, likinukuu Al-Ma'loomah, vikosi vya Hashd al-Sha'abi vilifanikiwa kumkamata Abdul Razzaq Oudah, mmoja wa viongozi wakuu wa Chama cha Ba'ath kilichovunjwa, katika operesheni yao ya hivi karibuni ya kiusalama.
Kulingana na ripoti hiyo, operesheni hiyo ilifanyika baada ya kufuatilia kwa wiki kadhaa mienendo ya Oudah nchini Iraq kwa kutumia ujasusi. Alikuwa mmoja wa watu wenye ushawishi katika utawala wa zamani wa Iraq ambaye alihusika katika kufanya uhalifu dhidi ya taifa hilo, ikiwa ni pamoja na kunyong'onga watu wengi wasio na hatia.
Pia, imeripotiwa kuwa mtu huyu alifanya harakati dhidi ya usalama wa Iraq na alikuwa akishirikiana na viongozi wengine wa Chama cha Ba'ath kilichovunjwa kwa lengo la kuzua fitina nchini humo.
Vikosi vya Hashd al-Sha'abi vilitangaza kwamba hawatakubali chama hiki kurejesha Iraq tena katika kipindi kigumu cha zamani.
Your Comment